Katika kitabu
cha “Power of positive thinking” Na Vicent Peal kinaeleza kwamba kuna mfumo
miwili ya kufikiria. Kufikiria vibaya na kufikiria vizuri.
1.
Kufikiria vizuri
Kufikiria vizuri
ni kujaza akili zetu mambo ambayo ni mazuri na yenye kututia moyo. Ni kujaza
fikira zetu na matukio yenye matarajio na picha zenye kututia faraja na
matumaini. Matokeo ya kufikiria vizuri hupelekea mtu aweze kufikia malengo
aliyojiwekea katika maisha. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, utakuwa na
mtazamo chanya juu ya jambo lile unalotaka kulifanikisha katika maisha yako.
Kukatishwa tamaa kwako itakuwa vigumu kwani utakuwa na msimamo na Imani ya
kwamba kila kitu kinawezekana.
2.
Kufikiria vibaya
Kufikiria vibaya
ni kujaza akili zetu mambo yasiyofaa naya kukatisha tamaa, kuwaza ubaya,
ulipiza visasi, kinyongo, hasira, chuki, fitina na mambo mengine ya kufanana
kama hayo. Kwahiyo katika kufikiria kubaya amani, upendo, utulivu, kutenda haki
na furaha havipo. Matokeo ya kufikiria vibaya ni mtu kukata tamaa na maisha,
kumwona kila mtu ni mshirikina na mnafiki katika maisha. Na wakati mwingine
kufikiria vibaya hupelekea mtu kuchukia watu bila ya sababu za msingi.
Njia zinazoweza
kumsaidia mtu kufikiria vizuri.
1. Tusome,
kusikiliza na kutazama mazuri.
Vijana
waliowengi katika ulimwengu wasasa wa sayansi na teknolojia wamekuwa limbukeni
wa teknolojia. Matumizi ya simu na mitandao imebadilika, yanayofuwatiliwa na
mambo yanayopendwa zaidi ni mambo ya kipuuzi na ambayo si mazuri kabisa. Wengi
wamekuwa wafualitiaji wa umbeya na sababu za ndoa nyingi kuvunjika kwasababu
vitu wanavyoangalia kwenye mitandao, habari wanazopashana, hakika haziwafanyi
waweze kujadili mambo ya msingi katika maisha hivyo kupelekea kufikiria vibaya.
Matokeo ya kufikiria vibaya ni mambo ya aibu tunayoyaona katika jamii zetu,
yanayoposha ambayo hapo nyuma hayakuwepo. Hii hutokana na kuiga na kufuatisha
vile vijana wengine kutoka sehemu mbalimbali wanayoweka mitandaoni na kuiga
bila hata kujiuliza maswali. Hii hupelekea kufikiri kubaya.
Hivyo ili uweze
kufikiria vizuri hauna budi kutazama, kusoma na kusikiliza mambo mazuri ambayo
hukufanya uwe mtu fulani “somebody” katika maisha yako. Kinyume na hayo utakuwa
unaishi maisha ya watu wengine walioshindwa kwasababu ya kufikiria vibaya.
2. Tutumie
lugha nzuri katika mawasiliano.
Kadri siku
zinavyosogea katika jamii zetu ndivyo maadili yanavyozidi kuporomoka. Hii yote
hutokana na vizazi vipya “new generation” kufuatana na ulimwengu bila ya
kuangalia hasara na faida za kufuata ulimwengu huu wa leo. Maarufu kama
ulimwengu wa “dotcom (.com).” wananchi wengi hususan vijana wamekuwa wakitumia
lugha za matusi wanazozitoa katika miziki ya wasanii kutoka nchi zilizoendelea.
Hii imechangia sana kuporomoka kwa maadili ya vijana katika jamii zetu jambo
linalotishia kutokomeza kabisa ile asili yetu kabisa. Mtu anayetumia lugha
mbaya katika mawasiliano siku zote atawaza mabaya wala hataweza kuwaza jambo
jema hata siku moja. Kwahiyo tuangalie sana lugha tuzitumiazo katika masaliano
yetu.
3. Tuepuke
marafiki wenye fikira mbaya.
Marafiki ni watu
wazuri sana lakini kama haujaweza kuchagua marafiki vizuri; wanakuwa ni watu
wabaya sana kupita maelezo. Marafiki tunaoandamana nao kila siku, tunaoishi nao
na tunaofanya kazi nao wanaushawishi mkubwa sana katika tabia zetu. Ukiwa
rafiki wa mtu anayefikiria vibaya na wewe utakuwa mmoja wao. Kwani hauwezi
kujizuia kufikiria vibaya wakati katika mazungumzo mnayozungumza hakuna mtu
hata mmoja anayezungumza kitu cha maana. Kwahiyo ili uweze kufikiria vizuri ni
lazima ujitenge na marafiki au kundi la watu wanaofikiria vibaya na kujiunga na
watu wanaofikiria vizuri.
4. Tuwaze vitu
chanya badala ya vitu hasi.
Ukiandamana na
watu ambao kila kitu kwao wanaona hakiwezekani, usifikirie kwamba itafika siku
utafikiria kwamba jambo fulani linawezekana. Wala usitegemee kwamba usiwaza
kushindwa tu kila wakati basi itafika wakati ushinde. Kila wazo baya huzaa
uharibifu. Mawazo chanya ni kuona kwamba kila kitu kinawezekana, ni kujipa moyo
ili kufikia mafanikio uliyojipangia. Ni kuwa na maono na fikira yakinifu au
fikira pevu. Mtu mwenye kuwaza vitu chanya yuko tayari kuthubutu kufanya vitu
kwa ujasiri kwani anaamini katika uwezo alio umbwa nao.
5. Tukariri aya
zenye kutia moyo.
Kukariri aya
zenye kutia moyo hutokana nay ale tunayoyasoma na kusikia kutoka kwa watu
wengine. Kwa mfano maneno ya kutia moyo ambayo watu hupata kutoka makanisani na
misikitini yanaweza kukaririwa na mtu na hivyo kumfanya mtu husika kufikiria
vizuri. Aya zenye kutia moyo pia zinaweza kunukuriwa kutoka kwa watu maarufu na
mashuhuri walioshinda na kufanikiwa katika mambo waliyokuwa wanafanya. Hii
itamsaidia mtu aweze kufikiria vizuri na kufikia mafanikio anayohitaji katika
maisha yake.
No comments:
Write comments