Ni ukweli
usiopingika kwamba hauwezi kubadilisha jana, na haujui ya kesho; siku pekee
uliyonayo ni leo hivyo unaweza kuitumia vizuri leo na kubadirisha hatima yako
ya kesho. Wengi tumeshindwa kufanikiwa kwasababu ya kuangalia nyuma yale ambayo
yalitushinda na kukataa tamaa ya kujipanga upya. Tunasahau kwamba kuangalia ya
nyuma ambayo hatuwezi kuyarudisha au kurekebisha yanatufanya tuzidi kupoteza
muda wa kusonga mbele. Tunasahau kwamba hali za maisha tulizonazo sasa
hazihusiani kabisa na maisha ya baadae. Maisha yanabadilika kwahiyo usifikilie
kuwa na hali uliyonayo mpaka mwisho.
Fanya yafuatayo
ili kutoka katika hali uliyonayo kwenda hatua nyingine mbele kuelekea mafanikio
yako:-
1. Komboa
wakati.
Usipoteze muda
kuhesabu yale ambayo umeyapoteza, angalia ni wapi umejikwaa na wapi umeanguka
halafu inuka haraka sana kupiga hatua mbele kuelekea mipango yako. Usipoteze
muda kujifananisha na watu wengine kwani kila mtu ana njia zake za kufanikiwa
na hauwezi kufanya kama mwenzako alivyofanya kufanikiwa. Katika Biblia Waefeso 5:15-17 “Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima
bali kama watu wenye hekima; mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za
uovu. Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya
Bwana.” Tunaaswa kuwa na hekima katika kupangilia wakati, na kufahamu
mapenzi ya Mungu ambayo tumeona hapo juu kwamba Mungu anakuwazia mema.
Ukishajua hayo piga hatua mbele.
2. Jiimarishe
kila siku.
Inawezekana
hauendelei mbele kwasababu ya utendaji wako kuwa mbovu, au haujajipanga vizuri.
Hivyo kila siku jaribu kuangalia ni nini umekifanya kwa siku nzima na ujipange
kwaajiri ya siku inayofuata. Fanya mazoezi ili kuufanya mwili kuwa na nguvu na
afya njema, fanya yale yote mazuri unayoona hauyaweji, kidogo kidogo utazoea na
utakuwa imara.
3. Anzisha kitu
chenye maana katika maisha yako.
Kila kitu
unachoanzisha katika maisha yako au unachoamua kufanya hakikisha kwamba kina
manufaa katika maisha yako. Na kama haujaanzisha kitu chenye manufaa katika
maisha yako jaribu kuanzisha, taratibu kadri ya uwezo ulionao. Epuka kufanya
mambo au kuanzisha vitu katika maisha kwa kuiga watu wengine. Si kila kitu
nachokifanya mtu mwingine basi kitakuwa na maana kwako, kwahiyo usiige maisha
ya watu wengine.
4. Fanya mambo
yako kwa ubora wa hari ya juu.
Kila kitu
unachokifanya jaribu kufanya kwa ubora wa hari ya juu. Kwa mfano kama wewe ni
mjasiriamali na unafanya kazi sawasawa na wenzako. Jitahidi kujitofautisha nao
kwa kufanya kwa ubora zaidi. Kuwa mbunifu katika kile unachokifanya ili uweze
kuonekana bora kuliko watu wengine. Hii itakusaidia kupata wateja wengi zaidi,
au watu watapenda zaidi kuja kwako kupata hudumu hivyo kuchochea mafanikio
yako.
5. Kuwa mfano
kwa wengine.
Utakuwa mfano
kwa wengine kama utajitofautisha na wengine katika utendaji. Kama utendaji wako
ni mzuri basi kila mtu atakuwa anaufurahia. Na utakuwa mfano kwa kila mtu
atakayepata huduma kwako. Samahani kwa mfano huu “Mwendesha bodaboda mmoja
jijini Dar amekuwa akivaa kwa heshima anapokuwa katika kazi yake hiyo.
Anaendesha kwa ustarabu na amelipia kila kitu. Amefanikiwa katika kazi yake
hiyo kwani kila abiria anaepanda bodaboda yake, anafurahia huduma yake na
anatamani kila siku angempata. Hivyo watu wengi wamechukua namba yake ya simu,
na huwa wanamtumia sana.” Huyu ni mfano wa kuigwa na wenzake.
6. Kuwa tayari
kufanya maamzi.
Mara nyingi
tunakuwa tunasitasita kufanya maamzi kwa wakati mwafaka. Kuchelewa kufanya
maamzi au kuogopa kufanya maamzi humchelewesha mtu kufikia malengo yake. Kwa
mfano mtu anafanya kitu ambacho haoni faida yake lakini anang’ang’ana na kitu
hichohicho. Anaogopa kuacha na kujaribisha kufanya jambo jingine. Hii hupelekea
kushindwa kubadilika kabisa na hivyo kupeleke aendelee kuwa masikini na mtumwa
wa kazi anayong’ang’ana nayo.
7. Fikiria
jinsi ya kutatua matatizo.
Unatakiwa kujua
kwamba matatizo hayana budi kuja. Na kwamba kila tatizo lanalokuja katika
maisha yako hautakiwi kulikimbia. Katika kitabu cha “Power of positive Thinking
by Vicent Peal” kinasema katika kila tatizo linamkumba mwanadamu ndani yake
kuna suluhisho la tatizo hilo. Hivyo kama maandiko matakatifu yanavyosema
katika Yakobo 1:12 “Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha
kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.” Hatutakiwi
kukimbia matatizo au majaribu tunatakiwa kuafuta ufumbuzi wa matatizo hayo na
kupiga hatua mbele.
No comments:
Write comments