Subscribe us

Thursday, 28 July 2016

Kanuni kumi na mbili (12) za kufanikiwa katika maisha. 2


9.      Heshimu /tunza muda.
Muda ni zawadi ambayo Mungu alitoa sawa kwa kila mwanadamu. Kila mwanadamu ana masaa 24 kwa siku, hakuna mwenye chini wala juu ya hapo. Kwahiyo ipo faida ya kutunza muda na kuutumia vizuri. Hii ni kutokana na ukweli kwamba muda ukisha pita umesha pita na hauwezi kwenda nyuma.
Kugawanya muda na matukio au shughuli zako vizuri na kujitoa kwa moyo wote katika shughuli uzifanyazo hupelekea kufikia mafanikio. Kushindwa kufanya hivyo hupelekea kutofanikiwa kabisa katika maisha na siku zote muda utakuwa hautoshi na utajutia maamuzi uliyofanya katika kipindi kilichopita na muda uliopoteza.

   

1.  Panga bajeti kabla ya kufanya manunuzi.
Kabla ya kununua vitu ni vizuri kuviandika na kupiga hesabu yake kuepuka ufujaji wa pesa na kununua vitu ambavyo haujapanga kununua. Siku zote utambue kwamba kununua vitu ambavyo vinakuwa nje ya bajeti uliyopanga ni kukosa nidhamu katika matumizi ya pesa zako. Bajeti hukusaidia uwezekufanya manunuzi sahihi, na ile unayozidi baada ya kununua vitu kwa muhimu unaweza kutumia kununua mengineyo.

1.  Jiwekee malengo.
Siku zote kuwa na malengo, panga mambo ya kufanya baada ya kipindi fulani. Yaandike malengo yako katika karatasi (note book), anza na mpango mmoja mmoja kulingana na mahitaji kwa kipindi ulichonacho. Malengo unayoyapanga yaweze kubadilika na yasiwe yasiyo badilika kwani kipindi kingine unaweza ukashindwa kufikia malengo uliyojiwekea na kujikuta unarudia na kushindwa kila wakati. Lazima uwe na kitu kingine mbadala cha kufanya kama malengo ya mwanzo yasipofikiwa.

1.  Mtegemee Mungu siku zote na usizitegemee akilizako mwenyewe.
Siku zote katika mambo unayofanya ukumbuke kwamba kuna Mungu. Watu wengi wamekosa hekima katika shughuli wanazozifanya kwa sababu ya kukosa kumtegemea Mungu na badala yake kuzitegemea akili zao wenyewe. Biblia inasema katika
MITHALI 3:5-6 “Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako.”
Ukimtegemea Mungu katika kila jambo atakufanikisha, mambo yanaweza muda mwingine kuonekana hayaendi lakini ukimtegemea Mungu atakupa hekima na akili ya kufanya maamzi ya mambo yako ili kufikia malengo yako.


No comments:
Write comments

Hey, we've just launched a new custom color Blogger template. You'll like it - https://t.co/quGl87I2PZ
Join Our Newsletter